Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:00

Ban Ki Moon kuzuru DRC


Katibu mkuu wa umoja mataifa Ban Ki Moon.
Katibu mkuu wa umoja mataifa Ban Ki Moon.

Ban Ki Moon atarajiwa kuwatembelea watu waloathiriwa na mizozo ya kibinadam nchini DRC.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ,anatarajiwa kuzuru mji wa Goma, huko mashariki mwa amhuri ya kidemokrasi ya Congo, mnamo tarehe 23, Februari. Bw. Ban kadhalika, anatarajiwa kuwatembelea watu waloathiriwa na mizozo ya kibinadam na hali ya ukosefu wa usalama katika eneo hilo, na vilevile kuwatembelea watu walopoteza makazi yao wanaoishi kwenye kambi nchini humo.

Ziara ya Bw. Ban italenga kutathmini shughuli ambazo ujumbe wa walinda amani wa Umoja Mataifa nchini Congo, MONUSCO, wamekuwa wakifanya.

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja Mataifa wamekuwa nchini DRC, wakifanya juhudi za kuleta amani katika eneo la Mashariki mwa Congo, ambako kwa mda mrefu raia wamekuwa wakilalamika kuhusu hali mbaya ya kiusalama, hasa kutokana na waasi kutoka Rwanda wa FDLR katika eneo la Lubero na Walikale, ambao wamekuwa wanatuhumiwa kufanya vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadam, pamoja na waasi wa Uganda wa ADF katika eneo la Beni, Kivu kaskazini.

Katibu Ban Ki Moon, pia anatarajiwa kuhudhuria kikao cha ufunguzi cha mkutano wa kanda ya maziwa makuu wa uwekezaji katika sekta binafsi ambao utafanyika mjini Kinshasa tarehe 24-25 Februari, na pia anapanga kukutana na rais Joseph Kabila na wanaharakati wa DRC.

XS
SM
MD
LG