Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:49

Trump awabeza wapinzani wake kuvuruga mchakato wa kuwania urais


Mrepublican Donald Trump akiwasili kwenye moja ya mikutano ya kampeni.
Mrepublican Donald Trump akiwasili kwenye moja ya mikutano ya kampeni.

Bilionea Donald Trump ambaye anaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kupitia chama cha Republican amewabeza wapinzani wake wawili kutaka kuvuruga juhudi zake na kusema hatua hiyo " ni kitendo cha hali ya kukata tamaa".

Wapinzani wa Trump, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Gavana wa Ohio, John Kasich, wametangaza mpango huo Jumapili usiku kujaribu kumnyima fursa Trump, ambaye hawajahi kushika wadhifa wa kuchaguliwa, ili asishinde uteuzi katika upigaji kura wa kwanza wa chama utakaofanyika kwenye mkutano wa ktiaifa wa Republican mwezi July, kwa matumaini kuwa wajumbe watawachagua wao katika upigaji kura utakaofuata.

Trump amekejeli juhudi za Cruz na Kasich akisema, "inasikitisha sana kwamba wanasiasa wawili watu wazima wanapanga dhidi ya mtu mmoja ambaye amekuwa mwanasiasa kwa miezi 10 tu ili kujaribu kumzuia mtu hiyo kupata uteuzi wa Republican."

XS
SM
MD
LG