Seneta wa texas Ted Cruz amejitoa katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa tiketi ya Republican baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali dhidi ya mpinzani wake bilionea muuzaji wa nyumba Donald Trump jana jumanne .
Cruz aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Indianapolis kwamba “ njia hii kuelekea ushindi imefungwa” na kusema kuwa wapiga kura wamechagua njia nyingine.
Alitoa shukrani kwa wafuasi wake wote . Trump alipata ushindi mkubwa Indiana jana huku Cruz akishika nafasi ya pili na gavana wa Ohio John Kasich akiwa katika nafasi ya tatu.
Trump amesema kwake huo ni ushindi mkubwa na akampongeza Cruz akimwita yeye na wagombea wengine 15 waliokuwa wanagombea uteuzi wa republican kuwa ni werevu na wenye nguvu.
Ametoa wito wa kuwa na umoja ndani ya chama cha republican. Kwa upande wa democrat seneta wa vermond Bernie Sanders ameshinda katika jimbo la Indiana dhidi ya Hillary Clinton.
Wagombea hao wawili walibadilishana ushindi usiku wa jana kabla ya Sanders kuibuka mshindi kwa asilimia 7 ya kura. Hata baada ya ushindi huo wa sanders katika jimbo la Indiana, Clinton anaongoza katika idadi ya wajumbe ikionyesha kwa mahesabu ni vigumu kwa Sanders kuteuliwa kuwa mgombea wa Democrat .
Facebook Forum