Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 04:51

Dola milioni 115.7 zatolewa kwa ajili ya kutoa chanjo za Malaria Afrika


Mfanyakazi wa afya wa Kenya ajiandaa kutoa chanjo ya Malaria kwa watoto

Muungano wa chanjo ulimwenguni wa Gavi Alhamisi umesema kwamba bodi yake imeidhinisha dola milioni 155.7, kuelekea zoezi la utoaji wa chajo za kwanza za malaria kwa watoto kwenye mataifa yalioko chini ya jangwa la Sahara barani Afrika. 

Mwenyekiti wake Jose Manuel Barroso ameeleza kufurahishwa na hatua ya bodi yake akiongeza kwamba hilo limewezekana kupitia juhudi za pamoja za jamii ya kimataifa ya afya, na kwamba zoezi hilo litakapoanza, basi litaokoa mamilioni ya maisha ya watoto.

Mwezi Oktoba shirika la afya duniani WHO liliidhinisha chanjo ya kwanza ya malaria, ili kupambana na maradhi hayo yanayosababishwa na mbu, na ambayo hupelekea zaidi ya vifo 400,000 kila mwaka hasa barani Afrika, miongoni mwa watoto.

Kumekuwepo na chanjo aina nyingine za malaraia lakini hiyo kwa jina RTS.S ndiyo ya kwanza kupendekezwa na WHO kutumika kwa umma dhidi ya malaria. Fedha zilizoidhinishwa zitatumika kwa kuagiza na kusafirisha chanjo hizo pamoja na hatua nyingine za kuzuia maambukizi kama vile neti za mbu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG