Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:17

Wademokrat wakusanyika Philadelphia


DNC 2016
DNC 2016

Wademokrat nchini Marekani wameanza kukusanyika Jumapili katika mji wa Philadelphia, tayari kwa mkutano mkuu wa chama hicho utakaofikia kilele kwa kumteua Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Hillary Clinton kama mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa Novemba. Itakuwa mara ya kwanza kwa chama cha siasa Marekani katika historia kumteua mwanamke katika nafasi hiyo.

Mkutano huo unaanza Jumatatu huku kukiwa na shutuma kwamba viongozi wa chama hicho walimcheka na kumdhihaki Seneta Bernie Sanders ambaye alikuwa akiwania ugombea dhidi ya Clinton.

Barua pepe zilizovujishwa na mtandao wa wikileaks zinaonyesha kuwa viongozi walikuwa wakimsema Sanders na moja ikiiuliza endapo Sanders anaamini mungu, ingawa inajulikana kuwa ni muumini ya dini ya kiyahudi.

Katika mahojiano na shirika la televisheni la CNN, Sanders alisema barua hizo zinasikitisha lakini hazikumshangaza kwa sababu kampeni yake ilijua kuwa chama hicho kinamwunga mkono Clinton katika uchaguzi wa awali.

Sanders amekwishatangaza kumwunga mkono Clinton na atazungumza katika mkutano huo Jumatatu na anasema “atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa” Donald trump hashindi uchaguzi wa Novemba.

Miongoni mwa wazungumzaji wa Jumatatu katika mkutano huo wa wademokrat atakuwa Michelle Obama, mke wa rais wa sasa Barack Obama ambaye pia ametangaza kumwunga mkono Hillary Clinton.

XS
SM
MD
LG