Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 04:00

Dlamini-Zuma mwenyekiti mpya wa AU


African leaders pose for a group photograph with U.N. Secretary-General Ban Ki-moon during the 18th African Union summit
African leaders pose for a group photograph with U.N. Secretary-General Ban Ki-moon during the 18th African Union summit

Nkosazana Dlamini-Zuma anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza umoja huo tangu kuanzishwa mwaka 1963.

Bi Dlamini-Zuma ambae ni waziri wa mambo ya ndani wa Afrika Kusini anakuwa mwenyekiti mpya wa AU baada ya kumshinda Mwenyekiti wa sasa Jean Ping wa Gabon, baada ya duru nne za uchaguzi Jumapili.

Alipata kura 37 za viongozi wa Arika katika kura ya siri iliyofanyika kwenye makao makuu ya AU, akipata theluthi mbili zinazohitajika kushika nafasi hiyo.

Rais wa Benin, Boni Yayi ambae ndiye rais wa zamu wa AU alipongeza matokeo hayo.

"Hivi sasa tuna rais wa Baraza la Utawala la AU Bi. Zuma ambae ataongoza mustakbal wa taasisi hii yetu".

Dlamini-Zuma na mwenyekiti wa AU anaeondoka Jean Ping walipigania nafasi hiyo wakati wa mkutano uliyopita wa viongozi mwezi Januari, lakini hakuna mgombea aliyepata kura za kutosha kuweza kutangazwa mshindi.

Dlamini–Zuma ambae ni mke wa zamani wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma atakua mwanamke wa kwanza kuongoza umoja huo na mwafrika kusini wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uchaguzi Bi.Dlamini-Zuma alisema kwamba akichaguliwa atatumia siku zake za kwanza madarakani kutafakari jinsi atakavyo imarisha kazi za AU.

"Sidhani mchango wangu utahusu kufanya mambo tofauti na aliyenitangulia. Lakini mchango wangu ningelipenda uwe kuuchunguza umoja huu na kuona jinsi nitakavyo imarisha kazi zake ili ifanye kazi kwa ubora, ustadi na utahbiti zaidi".

Tangu mwanzo, pale Dlamini-Zuma, alipotangaza kugombania nafasi hiyo kulizuka utata katika Umoja huo kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kwa maridhiano kwamba viongozi kutoka mataifa makuu ya bara hilo hawatoweza kuiongoza AU. Bi. Dlamini-Zuma anasema haoni kama kutakua na tatizo lolote sasa amechaguliwa

Anachukua nafasi hiyo wakati bara la Afrika linakabiliwa na mizozo mbali mbali ikiwa ni pamoja na uwasi wa wanaharakati wa kislamu kaskazini ya Mali na uwasi mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Mkutano huo wa viongozi ulipofunguliwa Jumapili asubuhi viongozi walitoa wito wa kuitaka AU kuwa na jukumu kubwa zaidi katika kutatua migogoro ya kikanda. AU ina mipango ya kusaidia kijeshi huko mashariki mwa DRC na Mali.

XS
SM
MD
LG