Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:24

Dhoruba ya theluji yakata umeme Ukraine


Wafanyakazi wa dharura wakikuamua gari kutoka kwenye dheluji kwenye eneo la Odesa region, Ukraine Nov. 27, 2023.
Wafanyakazi wa dharura wakikuamua gari kutoka kwenye dheluji kwenye eneo la Odesa region, Ukraine Nov. 27, 2023.

Wakati kukiwa na wasiwasi wa mashambulizi yanayofanywa na Russia wakati wa majira ya  baridi, mfumo wa  usambazaji umeme wa Ukraine leo Jumatatu umepata pigo kutokana na  dhoruba ya theluji.

Hali hiyo imesababisha kukatika kwa umeme na kuathiri utoaji wa huduma hiyo kwa zaidi ya miji elfu mbili pamoja na vijiji nchini humo. Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema kwamba miji kwenye mikoa 16 haina umeme kutokana na dheluji, wakati maeneo ya kati na kusini mwa nchi yakiwa yameathiriwa zaidi.

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy wakati wa hotuba yake ya kila siku kwa taifa Jumapili usiku, alichukua nafasi hiyo kuwashukuru wafanyakazi waliokuwa wakijitahidi kurejesha huduma hiyo. Aliongeza kusema kwamba wakati wa kipindi kigumu kama hicho, watu wa Ukraine wanahitaji kuwashukuru wanajeshi wanaokabiliana na uvamizi wa Russia.

Mwaka uliopita wakati wa msimu wa baridi, Russia mara kadhaa ilishambulia mfumo wa umeme wa Ukraine na kusababisha kupotea kwa umeme kwenye sehemu nyingi za taifa.

Forum

XS
SM
MD
LG