Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:59

Spiegel yaeleza chanzo cha ajali ya ndege ya Ujerumani


Ndege aina ya Airbus Tiger
Ndege aina ya Airbus Tiger

Jarida la kijerumani la Der Spigel kwenye mtandao liliripoti Jumanne kwamba kuanguka kwa ndege ya kijeshi aina ya Airbus Tiger ya jeshi la Ujerumani limetokana na sababu za kiufundi.

Ajali hiyo ilitokea huko nchini Mali mwezi Julai 2017, na wataalamu wanasema kuwa ilisababishwa na kukosekana utaratibu sahihi wa mfumo wa ndege wa kujiendesha yenyewe.

Ndege hiyo ilianguka wakati ikisafiri na ujumbe wa kulinda Amani kuelekea eneo la kaskazini la jangwa la taifa hilo la Afrika magharibi na kuwauwa wafanyakazi wawili.

Der Spiegel liliandika wizara ya ulinzi iliarifu kamati ya ulinzi bungeni kuhusu uchunguzi mpya uliopatikana Jumanne. Ilisema utaratibu wa ndege kujiendesha yenyewe ulidhibiti ndege kupaa juu na haijafahamika bado ni nani alipanga utaratibu huo kwenye kompyuta ya ndege hiyo ambao haupo katika ndege nyingine za Tiger.

XS
SM
MD
LG