Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:16

Majadiliano kuhusu Ugiriki yapiga hatua


Greece's Prime Minister Alexis Tsipras addresses lawmakers on a controversial austerity bill during a parliamentary session in Athens, May 8, 2016.
Greece's Prime Minister Alexis Tsipras addresses lawmakers on a controversial austerity bill during a parliamentary session in Athens, May 8, 2016.

Mawaziri wa Fedha wa Umoja wa Ulaya wanasema kuwa wamepiga hatua kubwa katika majadiliano yao kuhusu makubaliano ya kupunguza deni la Ugiriki, baada ya mazungumzo ya saa kadhaa yaliyofanyika jana usiku mjini Brussels, Ubelgiji.

Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeitaka Ugiriki kupunguza mzigo wake wa deni kama sharti ya kutoa fedha zaidi za IMF kuokoa uchumi wa nchi hiyo.

Ugiriki itapokea sehemu ya kwanza ya mkopo wa kuinusuru wa dola bilioni 11.4 mwezi Juni, kufuatia kuidhinishwa kwa juhudi za mageuzi za karibuni zilizofanywa na taifa hilo.

Huu ni mkopo mpya katika kitandawili cha miaka sita ya matatizo ya kiuchumi inayoikumba Ugiriki na kupelekea deni kubwa ambalo ni asili mia 180 ya pato la kitaifa.

XS
SM
MD
LG