Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:51

David Cameron waziri mkuu mpya Uingereza


Uingereza ina Waziri Mkuu mpya. Ni David Cameron, kiongozi wa chama cha Conservatives ambacho kilipata kura nyingi kuliko vyama vingine katika uchaguzi wa wiki iliyopita.

Uingereza ina Waziri Mkuu mpya. Ni David Cameron, kiongozi wa chama cha Conservatives ambacho kilipata kura nyingi kuliko vyama vingine katika uchaguzi wa wiki iliyopita.

Hatua hiyo imefuata baada ya Bwana Cameron kukubaliana kuunda serikali ya mseto na kiongozi wa chama cha Liberal Democrats Nick Clegg, ambacho kilikuwa cha tatu katika uchaguzi. Waziri Mkuu wa zamani Gordon Brown wa chama cha Labour alitangaza kujiuzulu muda mfupi baada ya wapinzani wake hao kubaliana kuunda serikali mpya.

Baada ya tangazo lake leo nje ya ofisi ya waziri mkuu huko London Bw. Brown alikwenda Burkingham Palace na kuwasilisha kujiuzulu kwake kwa Malkia wa Uingereza.

Conservatives walishinda viti vingi katika uchaguzi wa wiki iliyopita wa bunge ingawa si wa kutosha kuweza kutawala peke yao. Walikuwa wakifanya mazungumzo na Liberal Demokrats katika mpango wa kushirikiana madaraka.

Bw. Brown anamaliza miaka 13 ya uongozi wa chama cha Labor.

Bw. Brown alisema awali kuwa angejiuzulu wakati chama chake pia kilijaribu kupata muafaka na Liberal demokrats ambao walichukua nafasi ya tatu katika uchaguzi wa bunge. Mazungumzo kati ya Liberal democrats na Chama cha Labor yalishindikana mapema Jumanne.

Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu mwaka 1974 ambao umeacha Uingereza bila mshindi wa wazi.

XS
SM
MD
LG