Kundi la Wamorocco waliingia katika eneo la Melilla nchini Uhispania usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, kundi la haki za binadamu lilisema, kati ya darzeni kadhaa waliojaribu kuvuka katika moja ya mipaka miwili ya ardhi ya Umoja wa Ulaya na Afrika.
Darzeni ya vijana wa Morocco walijaribu kuvuka kuingia Melilla kutoka mji wa mpakani wa Nador siku ya mkesha wa Mwaka Mpya, Shirika la Haki za Kibinadamu la Morocco (AMDH) lilisema kwenye Twitter.
Watu kadhaa waliingia kwa mafanikio licha ya kuwepo kwa polisi katika eneo hilo ilisema taarifa ya shirika hilo katika eneo hilo la Uhispania.
Hakukuwa na uthibitisho wa haraka kutoka kwa mamlaka ya Morocco au Uhispania.