Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:50

Daktari wa mifugo aliyeshikiliwa mateka nchini Chad ameachiwa huru


Jerome Hugonnot, daktari wa kifaransa mwenye asili ya Australia azungumza baada ya kuachiliwa huru mjini N'Djamena
Jerome Hugonnot, daktari wa kifaransa mwenye asili ya Australia azungumza baada ya kuachiliwa huru mjini N'Djamena

Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby ametangaza kuachiliwa kwa Jerome Hugonnot siku ya Jumapili katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter bila kutoa maelezo zaidi

Mwana mazingira na daktari wa mifugo mwenye uraia pacha wa Ufaransa na Australia aliyetekwa nyara wiki iliyopita nchini Chad ameachiliwa huru.

Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby ametangaza kuachiliwa kwa Jerome Hugonnot siku ya Jumapili katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter bila kutoa maelezo zaidi.

Hugonnot ambaye anasimamia hifadhi ya oryx kwa niaba ya Mfuko wa Hifadhi wa Sahara, (SCF) alitekwa nyara Ijumaa na watu wasiojulikana.

SCF imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mingi kuwaingia tena wanyama aina ya swala katika mazingira ya jangwani wanaojulikana kama oryx wenye pembe za kisayansi.

Sababu ya kutekwa nyara kwa Hugonnot au kama fidia ililipwa kwa ajili ya kuachiliwa kwake haikuwekwa wazi mara moja.

XS
SM
MD
LG