Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 02:10

COVID-19 : ICU Hospitali ya Kenyatta yafurika wagonjwa


COVID-19 : ICU Hospitali ya Kenyatta yafurika wagonjwa
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:21 0:00

Baada ya wimbi la hivi karibuni la maambukizi ya COVID-19 nchini Kenya, vitanda katika kitengo cha wagonjwa mahtuti (ICU) cha Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, hospitali kubwa ya umma kuliko zote katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, vimejaa wagonjwa.

Huku ndiko kuelemewa kwa mfumo wa afya, wakati mwengine kitanda kwa mgonjwa mpya kinaweza kupatikana “wakati mgonjwa anapokufa” katika ICU, anaeleza Dkt Samuel Njenga, mtaalam bingwa wa magonjwa ya kuambukiz katika Hospitali ya Taifa ya Kenya.

Njia pekee ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaohitaji kupelekwa ICU ni kudhibiti idadi ya watu wanaoambukizwa na virusi, amesema.

Idadi ya maambukizi ya kila siku nchini Kenya imepungua kidogo tangu ilipokuwa juu katikati ya mwezi Machi, ilipokuwa imerekodi idadi rasmi ya juu kuliko zote tangu janga hilo kuanza.

Kwa ujumla nchi imeripoti zaidi ya maambukizi 147,000, ikiwemo zaidi ya vifo 2,300 vinavyo husishwa na COVID-19, kwa mujibu wa hisabu iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.Facebook Forum

XS
SM
MD
LG