Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 05:09

DRC yasherehekea miaka 50 ya uhuru


Wanawake Kivu Kusini wakisubiri huduma za matibabu. Sehemu nyingi za DRC wanawake wanakabiliwa na hatari ya kubakwa.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yafanya sherehe kubwa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaadhimisha miaka 50 ya uhuru leo Juni 30 kwa sherehe kubwa ambazo zimehudhuriwa na viongozi kadha kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Mfalme Albert wa pili wa Ubelgiji ambayo ilitawala Congo. Mfalme huyo wa Ubelgiji ni kiongozi wa kwanza kutoka katika ufalme wa nchi hiyo kutembelea Congo katika kipindi cha miaka 25. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia ni miongoni mwa wanaohudhuria sherehe hizo.

Viongozi wengine kadha wa Afrika ikiwa ni pamoja na nchi za jirani kama vile Paul Kagame wa Rwanda pia wanahudhuria sherehe za kitaifa katika mji mkuu Kinshasa.

Sherehe hizo zinafanyika huku Congo ikiwa inakabiliwa na changamoto mbali mbali. Ingawaje nchi hiyo ina akiba kubwa ya madini kama vile dhahabu, almasi na shaba, ni moja ya mataifa masikini sana duniani.

Congo bado ina machungu ya historia ngumu, iliyokuwa na utawala wa kikatili wa Mfalme wa zamani wa Ubelgiji Leopold, mauaji ya kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, Patrice Lumumba, utawala wa kidikteta wa Mobutu uliodumu kwa miaka 32, na vita ya hivi karibuni iliyosababisha vifo vya watu wapatao millioni tatu.

Umoja wa Mataifa una walinzi wa amani elfu 20 nchini humo, idadi kubwa kuliko duniani. Hata hivyo, Rais wa DRC Joseph Kabila anataka walinzi hao wa amani waondoke Congo ifikapo mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG