Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:44

New York washangilia ushindi wa Clinton na Trump


Mgombea wa chama cha demokrat Hillary Clinton, akishangilia ushindi wake na familia yake , kutoka kushoto, Chelsea Clinton, Mark Mezvinsky, na mme wake rais wa zamani Bill Clinton, baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa awali huko New York .Ap
Mgombea wa chama cha demokrat Hillary Clinton, akishangilia ushindi wake na familia yake , kutoka kushoto, Chelsea Clinton, Mark Mezvinsky, na mme wake rais wa zamani Bill Clinton, baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa awali huko New York .Ap

Jengo la 'Empire State' lilibadilika ilipofika saa 3 na dakika 45 jana usiku kwanza ilikuwa nyekundu ghafla ikabadilka kuwa blue. Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani, Bi. Hillary Clinton, alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa awali wa kinyanga’anyiro cha urais katika jimbo la New York. Jimbo alilohudumia kama seneta kwa miaka 8.

Ndani ya Sheraton Hotel huko New York karibu na eneo la Times Square kelele zilikuwa nyingi mno.

Kwa dakika mbili kundi la watu lilimshangilia shujaa wao wa nyumbani kwa muda ilionekana ameshinda kila kitu. Wakiimba “Madame President.”

“Mmefanya jambo bora sana kwa Marekani usiku huu" alitangaza meya jiji la New York, Bill de Blasio, kwa furaha kubwa mbele ya umati wa watu.

“Mlikuwa na nafasi moja na mnajua nini? Mmeitumia vizuri."

“Uso wangu una maumivu kutokana na kupiga kelele" alisema Kelly Kollar wakati akitoka hotelini.

Kollar alifurahi sana kumwona Clinton akishinda mgombea anayemwita mwenye busara, upendo na anayefaa. "Inasikitisha kidogo wakati mwingine akiona kama vile msisimko uko kwa Bernie na nafikiri usiku huu ulikuwa wa furaha sana kwangu kuweza kumshangilia Hillary na kuona kwamba msisimko umerudi kwake," alisema.

Hatua chache kutoka hapo katika mtaa wa tano nje ya Jengo la Trump Tower kulijaa magari ya waandishi wa habari na walinzi na polisi na kundi dogo la waandamanaji walisimama mbele ya duka la Prada.

Huku sherehe ziliendelea kwa wafuasi wa Donald Trump wakielekea mitaani kuchukua usafiri wa taxi kurudi majumbani mwao. Carl Paladino, mgombea nafasi ya ugavana wa New York na mwenyekiti wa kampeni za Trump huko New York, alifurahishwa na matokeo ya New York na kueleza kwa nini anamuunga mkono Trump akisema ni mkweli, mwaminifu na ni Donald Trump na atakuwa rais ajaye wa Marekani.

Sean, mkazi mwingine wa New York, ambaye alipiga kura mapema siku hiyo anasema Donald anawakilisha mabadiliko ya kweli yaliohitajika si mwanasiasa, nakubaliana na sera zake nyingi na kwa kweli Washington inahitaji mabadiliko makubwa.

XS
SM
MD
LG