Mgombea urais anayeongoza wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda majimbo matatu katika upigaji kura wa awali uliofanyika Jumanne ikiwemo jimbo muhimu la Florida na kumsababisha Seneta wa jimbo hilo Marco Rubio kujitoa katika kinyang’anyiro cha kampeni za urais na hivyo kujiongezea wajumbe mbele ya seneta wa Texas, Ted Cruz.
Jimbo pekee ambalo Trump alishindwa katika uchaguzi huo wa Jumanne ni Ohio, ambapo Gavana John Kasich alipata ushindi mkubwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lake. Bilionea mfanyabiashara Trump, alishinda jimbo la Florida kwa wingi wa asilimia 19, lakini ushindi wake wa kiasi katika jimbo la North Carolina na Illinois, ulimsaidia Cruz kupata wajumbe zaidi kwenye siku hiyo.
Trump na Cruz pia walifungana katika kinyang’anyiro hicho kwenye jimbo la Missouri. Hivi sasa kinyang’anyiro hiki kimebaki kwa Ted Cruz na Donald Trump wa Republican ambapo wote wanatoa wito wa chama kuungana pamoja. Kwa upande wa wademokrat Hillary Clinton alipata ushindi muhimu wa majimbo manne kati ya matano.
Profesa wa chuo kikuu cha Georgia Athens Dr.Lioba Moshi amezungumza na VOA akieleza kwamba uchaguzi huo umechukua sura mpya kwa chama cha republican kwa sasa kwa sababu njia yake haiko wazi pamoja na kuongoza chama chake kwasababu upande mmoja wa chama chake asilimia 60 ya wananchi waliofanyiwa uchunguzi wansema hawamuungi mkono.
Na katika mkutano mkuu wa chama cha Republikan huko Cleveland kutakuwa na sokomoko kubwa anaongeza Dr.Lioba kwasababu wanaweza warepublikan wa wapinzani wa Trump wanaweza wasijitoe mpaka mwisho na kuendelea kumpinga ambapo upigaji kura unaweza kufanyika tena.