Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 16:10

Trump akataa kusema kama atakubali matokeo ya uchaguzi


Mdemocrat Hillary Clinton na Mrepublican Donald Trump katika mdahalo wa mwisho Jumatano usiku.
Mdemocrat Hillary Clinton na Mrepublican Donald Trump katika mdahalo wa mwisho Jumatano usiku.

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump ameendeleza matamshi yake anayotoa kwenye kampeni ya kuwa utaratibu wa uchaguzi una wizi dhidi yake na kuyabainisha hayo katika mdahalo wa Jumatano usiku akikataa kusema kama atakubali matokeo ya uchaguzi wa Novemba 8.

“Nitaliangalia hilo wakati utakapofika,” amesema Trump.

Ameongezea kwamba anaamini kuwa vyombo vya habari vimepandikiza “sumu” kwenye vichwa vya wapiga kura dhidi yake na kwamba mpinzani wake, Mdemocrat Hillary Clinton, asingeruhusiwa kuwania urais.

Richard Herrera, profesa msaidizi katika chuo kikuu cha Arizona katika idara ya siasa na masuala ya ulimwengu, amesema taarifa ya Trump”haikubaliki” hata kidogo kutolewa na mgombea kutoka chama kikuu na huenda akawatia khofu wapiga ambao bado hawajaamua wampigie nani.

“Hiyo ni kuhoji uhalali wa mfumo wetu wa kisiasa, ambao sidhani kuwa watu wanaweza kukubali hilo,” Herrera ameiambia VOA. “Huenda wasiwe wanaipenda serikali kiasi hicho, wakati ambapo uaminifu kwa serikali ni mdogo, lakini kwa kweli hawatahoji hilo kama kura zao hazina maana.”

XS
SM
MD
LG