Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:31

Clinton na Trump wanaendelea kutupiana vijembe katika kampeni


Wagombea kiti cha rais wa Marekani, Donald Trump na Hillary Clinton wakikosolewa na vyombo vya habari vya China
Wagombea kiti cha rais wa Marekani, Donald Trump na Hillary Clinton wakikosolewa na vyombo vya habari vya China

Wagombea urais Marekani, Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democratic wanatupiana maneno kila mmoja akimmwambia mwenzake hafai kuwa rais wa Marekani katika siku za mwisho za kampeni kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumanne ijayo.

Trump anadai kuchaguliwa kwa Clinton kutaleta matatizo ya kikatiba wakati akielekea kwenye mikutano mitatu ya kampeni Jumatano katika jimbo la Florida, jimbo muhimu kwenye uchaguzi na anaeleza kwamba hawezi kupoteza ushindi jimboni humo na kuingia White House.

Donald Trump
Donald Trump

Mgombea huyo bilionea pia alisema Clinton atachunguzwa kama rais kutokana na namna alivyoshughulikia nyaraka za usalama wa taifa kwenye barua pepe zake binafsi wakati alipohudumu kwa miaka minne kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Wakati huo huo Clinton akiwa kwenye kampeni huko jimboni Florida alimshambulia Trump namna anavyowadhalilisha wanawake kwa miaka mingi kama ambavyo kampeni yake ilivyotoa tangazo jipya linaloelezea matamshi machafu ya kuwadhihaki wanawake kwenye mkanda uliorekodiwa mwaka 2005 na kujigamba kwamba angeweza kuwafanyia chochote kwa sababu yeye alikuwa mtu maarufu.

XS
SM
MD
LG