Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 04:39

Clinton na Sanders wafanya kampeni pamoja Jumanne


Hillary Clinton akiwa na Sanders wakijiandaa kwa kampeni ya pamoja Jumanne.

Mgombea urais wa chama cha Democrtaic Hillary Clinton atakua na mkutano wa kampeni Jumanne pamoja na seneta wa Vermont, Bernie Sanders, mpinzani wake mkubwa ndani ya chama chao katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa chama katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Tukio hilo kwenye jimbo la kaskazini mashariki la New Hampshire linafanyika wiki moja tu baada ya Clinton kumkaribisha kiongozi mwingine wa juu wa chama katika juhudi za kampeni yake Rais Barack Obama na kuwa pamoja kwenye jukwaa ili kumuunga mkono katika jimbo la kusini la North Carolina.

Clinton na Sanders walitoa taarifa ya pamoja ikieleza kuwa mkutano wa Jumanne utazingatia suala la kuijenga Marekani ambayo inanguvu ikiwa imeungana na uchumi ambao unafanya kazi kwa kila mtu na sio tu kwa wale walio juu.

Lugha hii inawakilisha vipaumbele vya kampeni za wote lakini hususan kwa Sanders anayejielezea kuwa ni mdemocrat msoshalisti ambae kwa kawaida anakosoa ushawishi wa matajiri kwenye siasa za Marekani wakati wote akiwa mgombea.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG