Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 00:38

Clinton na Sanders bado wanashindana kwenye majimbo ya uchaguzi yaliyobaki


Wagombea urais wa Democrat, Hillary Clinton (L) na Bernie Sanders.
Wagombea urais wa Democrat, Hillary Clinton (L) na Bernie Sanders.

Katika kinyang’anyiro cha urais Marekani ushindani wa uchaguzi wa awali unamalizika wiki hii katika jimbo lenye watu wengi nchini Marekani, la California.

Uchaguzi wa awali wa siku ya Jumanne utatoa jibu la swali pekee linalosubiriwa katika msimu wa uchaguzi wa awali wa kuwania urais mwaka huu kama Hillary Clinton au Bernie Sanders ndie atakuwa mteuliwa wa chama Democrat kuwania urais.

Kura za maoni zinaonesha kinyanga’nyiro kikali huko California jimbo ambalo Clinton na Sanders wanapigania kupata ushindi. Hata hivyo wote wanalenga nguvu zao kwa mpinzani wao Donald Trump mteuliwa wa Republican kwenye kinyang’anyiro cha urais.

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.

Mawazo ya Donald Trump sio tu tofauti, ni hatari hayaeleweki alisema Clinton akielezea sera zake za mambo ya nje wiki iliyopita. Sio tu hajajiandaa, ni kwamba hastahili kuchukua madaraka ambayo yanahitaji maarifa, uthabiti na wajibu mkubwa. Unafanya nini pale ambapo huna majibu ya kuhusu matatizo ya kweli, unawalaumu watu, alisema seneta wa Vermont, Bernie Sanders kwenye kampeni siku ya ijumaa. Hatuwezi kumruhusu Trump kutugawa.

Trump alijibu akikosoa utumiaji wa barua pepe binafsi wa Clinton akiwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani wakati wa utawala wa muhula wa kwanza madarakani wa Rais Barack Obama. Mfanyabiashara huto wa New York, alisema Ijumaa kwamba Hillary Clinton anatakiwa kwenda jela. Ninafikiri angetengeneza fedha nyingi kama angeandika hotuba na kuziuza kwa watu ambao hawapati usingizi.

XS
SM
MD
LG