Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Clinton atoa ushahidi wa shambulizi la Benghazi


Waziri wa zamani wa mambo ya nje Marekani, Hillary Clinton akisalimia watu kabla ya kuhojiwa bungeni, Oct. 22, 2015.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje Marekani, Hillary Clinton akisalimia watu kabla ya kuhojiwa bungeni, Oct. 22, 2015.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton alihojiwa Alhamis mbele ya kamati maalumu ya baraza la wawakilishi inayoongozwa na wa-Republican inayochunguza mashambulizi ya mauaji yaliyotokea mwaka 2012 kwenye ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi nchini Libya.

Bibi Clinton alikabiliwa na siku ndefu ya maswali kuhusu jukumu lake kabla na baada ya shambulizi la Septemba 11 kwenye eneo hilo, ambalo lilisababisha vifo vya balozi Christopher Stevens na wamarekani watatu wengine, wakati Clinton alipokuwa anashikilia nafasi ya mwanadiplomasia wa juu nchini Marekani.

Ushahidi wake unakuja wakati ukosoaji unao-ongezeka kufuatia shutuma kwamba wa-Republican wanatumia kigezo hicho kuharibu harakati za bi. Clinton za kupata uteuzi wa kuwania urais mwaka 2016 kupitia chama chake cha Democrat.

Wa-Democrat akiwemo bi. Clintom mwenyewe wamezima matamshi yaliyotolewa mwanzoni mwa mwezi huu na kiongozi wa walio wengi bungeni, Kevin McCarthy wakati alipoonekana kwenye kipindi kimoja cha televisheni ya Fox News ya Marekani. McCarthy alionekana akieleza kwamba tangu wabunge wa Republican walipounda kamati maalumu kuangalia kwa kina mashambulizi yaliyofanyika Benghazi, viwango vya ukusanyaji maoni kwa bi. Clinton vimeshuka.

Wafuatiliaji watakuwa wakiangalia kuona namna Clinton atakavyojibu maswali mbele ya kamati hiyo. Idadi ya kura za maoni zimeongezeka tangu alipoonekana kwenye mdahalo uliotangazwa nchi nzima wa mgombea urais wa Democrat, kigezo ambacho huwenda kilisaidia kupelekea Makamu Rais Joe Biden kutangaza kwamba hatoingia katika kinyang’anyiro cha kuwania urais.

Lakini mwenyekiti wa kamati hiyo, Trey Gowdy aliahidi katika mahojiano ya karibuni kwamba kuhojiwa kwa Clinton kutalenga juu ya hali ya usalama kwenye ubalozi mdogo mjini Benghazi katika miezi kabla ya mashambulizi.

XS
SM
MD
LG