Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 00:30

Cleveland Cavaliers ndio mabingwa wa NBA 2016


LeBron James wa Cleveland Cavaliers akishika kombe la ushindi huko Oakland, Calif., Jumapili, Juni 19, 2016.
LeBron James wa Cleveland Cavaliers akishika kombe la ushindi huko Oakland, Calif., Jumapili, Juni 19, 2016.

Timu ya Cleveland Cavaliers imechukua ubingwa wa NBA 2016 baada ya kuishinda timu ya Golden State Warriors (GSW) kwa pointi 93-89.

Ubingwa huo umeondoa ukame wa miaka 52 katika mji huo wa Cleveland ambao timu za mji huo zimejaribu kutafuta ybingwa kwa miaka kadhaa na kushindwa.

Pia imetoa wakati muhimu kwa Lebron James ambaye amekulia katika mji huo na kulazimika kuondoka kuelekea Miami ambako alishinda ubingwa mara mbili kabla ya kurudi nyumbani msimu uliopita .

Lebron James alishinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo (MVP) na baada ya mechi hiyo alisema "hii ni kwa ajili yenu Cleveland".

Timu hii imeweka historia kuwa ya kwanza kushinda baada ya kuwa nyuma kwa jumla ya michezo 3-1 katika fainali za NBA.

XS
SM
MD
LG