Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:53

Chinua Achebe afariki


Marehemu Chinua Achebe
Marehemu Chinua Achebe

Chinua Achebe alifahamika kama baba wa fasihi Afrika

Mwandishi mashuhuri wa riwaya kutoka Nigeria Chinua Achebe, ambaye wengi wanamfahamu kutokana na kitabu chake kwa jina “Things Fall Apart” ameaga dunia.

Kifo cha mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 82 kilitangazwa Ijumaa. Katika miongo mingi ya uandishi wa vitabu, Achebe anayesifika kama ‘baba wa fasihi Afrika’ aliandika riwaya nyingi pamoja hadithi zikielezea historia ya taifa lake la Nigeria.

Aliandika kitabu chake ‘Things Fall Apart’ katika miaka ya 20 kikielezea jinsi wazee wa kikabila wa Nigeria walivyosalimu amri mbele ya wakoloni wa Uingereza.Kitabu hicho kimetafsriwa katika lugha zaidi ya 50 na kuuza nakala milioni 8 kote duniani.

Achebe alipooza kutokana na ajali ya barabarani mwaka wa 1990 na ameishi Marekani kwa miaka mingi tangu wakati huo, akiendelea kutetea demokrasia katika nchi yake asili ya Nigeria.
XS
SM
MD
LG