Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 12:26

China yaongeza shinikizo dhidi ya Taiwan wakati uchaguzi wake ukikaribia


Picha ya sehemu ya mji mkuu wa Taiwan, Taipei. Januari 3, 2024.
Picha ya sehemu ya mji mkuu wa Taiwan, Taipei. Januari 3, 2024.

China imeongeza shinikizo dhidi ya Taiwan wakati kisiwa hicho kikielekea kwenye  uchaguzi wa rais na bunge wenye ushindani mkali hapo Januari 13, huku  ikisisitiza kwamba kuungana tena kwa kisiwa hicho na China ni lazima kufanyike, huku ikiongeza harakati  za kijeshi kuzunguka Taiwan.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kwamba juhudi za China za kuishinikiza Taiwan, zinaashiria mbinu za muda mrefu za China, ambapo kila kunapokuwa na uchaguzi, au kipindi baina ya uchaguzi,” Beijing hutumia mbinu ya kurubuni, kuwahadaa wakazi wa Taiwan.”

Hayo yamesemwa na J Michael Cole ambaye ni mshauri mkuu kutoka taasisi ya kimataifa ya Republikan inayokabiliana na ushawishi wa nje wa kidikteta, na yenye makao yake huko Taiwan, alipokuwa akizungumza na VOA. Wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya kwa taifa, rais wa China Xi Jinping alisisitiza kwamba kwa uhakika China na Taiwan zitaungana tena.

Forum

XS
SM
MD
LG