Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:20

China kupiga marufuku biashra ya pembe za ndovu mwishoni mwa 2017


Watawa wakibuda wakiwaombea ndovu walouliwa kutokana na shehena ya pembe zilizokamatwa Colombo Sri Lanka Jan 26, 2016
Watawa wakibuda wakiwaombea ndovu walouliwa kutokana na shehena ya pembe zilizokamatwa Colombo Sri Lanka Jan 26, 2016

Serikali ya China imetangaza kwamba itapiga marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwisho wa mwaka 2017.

Baraza la mawaziri la China katika taarifa yake hapo Ijuma, limeeleza kwamba “ili kulinda vyema ndovu na njia bora ya kupambana na biashara haramu China itasitisha hatua baada ya hatua viwanda na uuzaji wa pembe kwa ajili ya biashara, ifikapo mwisho wa 2017.”

Pembe za ndovu zilizokamatwa Colombo Sri Lanka mapema 2016
Pembe za ndovu zilizokamatwa Colombo Sri Lanka mapema 2016

China imekua ikikabiliwa na shinikizo kutoka Jumuia ya Kiamtaifa kukomesha utumiaji wa bidhaa za pembe. Na mwezi Machi baada ya mkutano kati ya marais Barack Obama na Xi Jinping, serikali ya Bejing ilieleza kwamba itapanua marufuku ya pembe na bidhaa za pembe zlizoagiziwa kutoka nje kabla ya 1975.

"Haya ni mabadiliko makubwa kwa ndovu wa afrika", alisema Aili Kang, mkurugenzi wa kitengo cha Asia cha Tasisi ya kulinda Wanyamapori iliyoko New York. “Nina fahari kubwa kwa nchi yangu kuonesha uwongozi ambao utasaidia kuhakikisha kwamba ndovu wana uwezo hivi sasa ya kunusurika na kutotoweka duniani.”

Shirika la habari la China Xinhua linaeleza kwamba marufuku hiyo itasababisha kufungwa kwa viwanda 34 na vituo 143 vya bishara vilivyoidhinishwa.

Biahsra ya peme ilipigwa marufuku 1989 na mkataba wa kimataifa chiniya shirika la CITES. China ndio soko kuu la duniani la biashara ya pembe za ndovu.

XS
SM
MD
LG