Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 16, 2026 Local time: 10:59

China inashutumiwa kutoa silaha kwa Russia kupigana Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin (kushoto) na rais wa China Xi Jinping (kulia) wakihudhuria maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa huhusiano wa kidiplomasia kati ya Russia na China
Rais wa Russia Vladimir Putin (kushoto) na rais wa China Xi Jinping (kulia) wakihudhuria maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa huhusiano wa kidiplomasia kati ya Russia na China

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Grant Shapps, ameshutumu China kwa kutoa msaada wa silaha kwa Russia kuendeleza vita vyake nchini Ukraine.

Shapps ameambia kongamano mjini Londona kwamba ujasusi wa Uingereza na Marekani umethibitisha kwamba China inatoa msaada wa silaha kwa Russia.

Amesema kwamba kuna haja ya kufuatilia swala hilo kwa karibu sana kwa sababu China imekuwa ikidai kwamba haina upendeleo katika vita hivyo.

Ubalozi wa China nchini Marekani ulisema mnamo mwezi uliopita kwamba China haijatoa silaha kwa Russia, na kuongezea kwamba sio China haihusiki na vita vinavyoendelea Ukraine.

Ubalozi wa China mjini London haujatoa taarifa yoyote kuhusu madai hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG