Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 12:45

Chile yaadhimisha miaka 50 tangu kufanyika kwa mapinduzi ya Pinochet


Jenerali Augusto Pinochet aliyekuwa Rais wa Chile kwenye picha ya 1977.
Jenerali Augusto Pinochet aliyekuwa Rais wa Chile kwenye picha ya 1977.

Rais wa Chile Gabriel Boric Jumatano ametetea vikali demokrasia wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi yalioongozwa na Jenerali Augusto Pinochet na kupelekea utalawa wa kidikteta wa kijeshi uliodumu kwa kwa karibu miongo miwili.

“Matatizo ya demokrasia yanahitaji kutatuliwa kwa demokrasia zaidi”, alisema Boric akiwa kwenye makao ya rais ya La Modena ambayo yalishambuliwa na ndege za kijeshi mwanzoni mwa mapinduzi hayo miaka 50 iliyopita. “Mapinduzi ya kijeshi au ukiukaji wa haki za binadamu kutoka kwa wale wanaofikiria tofauti hayakubaliki kamwe”, Boric alisema kwenye hotuba yake kwa taifa.

Hata hivyo watu wengi wa Chile wanaamini kwamba mapinduzi ya 1973 yalifaa, na kwamba Pinochet aliyekufa 2006 alikuwa kiongozi mwema aliyeleta maendeleo nchini Chile. Utawa wa Pinochet unafahamika kwa kukiuka haki za binadamu, kuuwa na kufunga wapinzani, pamoja na kutesa maelfu walioukosoa.

Zaidi ya watu 3,200 wanasemekana kuuawa na utawala huo huku wengine 1,469 wakitoweka. Miaka 50 baadaye, watu 297 wamehukumiwa kutokana na ukatili wa kibinadamu, wakati kesi dhidi ya wengine 1,300 zikiwa zinaendelea kusikilizwa.

Forum

XS
SM
MD
LG