Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la kibiashara la kila mwaka mjini Hannover, Scholz alimueleza rais wa Indonesia Joko Widodo, kwamba biashara kati ya mataifa yenye idadi kubwa ya watu Kusini mashariki mwa Asia pamoja na muungano wa mataifa EU, wenye mataifa wanachama 27, itakuza eneo la kiuchumi lenye watu milioni 700.
Kiongozi huyo wa Ujerumani ameongeza pia kwamba ana matumaini kwenye mazungumzo kati ya EU na muungano wa Mercosur wa Amerika Kusini, Mexico, Australia, Kenya na India. Ujerumani inajitahidi kupunguza utegemezi wa China kwenye bidhaa muhimu za kutengeneza vifaa vya kidijitali, pamoja na mpito kuelekea kwenye uchumi usiochafua mazingira.