Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:49

Chama tawala cha Botswana cha rudi madarakani


Wapiga kura wasubiri kupiga kura zao katika kituo cha kura cha Gaberone, Botswana, wakati wa uchaguzi mkuu Ijuma Okt 24.

Chama tawala cha Botswana chashinda tena katika uchaguzi.

Chama tawala cha Botwasa kimeshinda uchaguzi wa bunge Jumapili na kutoa nafasi kwa rais Ian Khama kuongoza muhula wa pili.

Chama cha Democratic, kilipata kura 29 dhidi ya 57 ya viti vya bunge vilivyokuwa vinashindaniwa.

Chama kipya kilichoundwa, umbrella for democratic change kimeshinda kwa nafasi ya pili kwenye uchaguzi na kuwa chama rasmi cha upinzani chenye takriban viti 12.

Bwana khama ni mtoto wa rais wa kwanza wa Botswana, Seretse Khama.

Chama cha Democratic kimeongoza nchi tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa muingereza.

Nchi hiyo inajulikana kama moja ya zile zenye demmokrasia imara katika bara la Afrika.

XS
SM
MD
LG