Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 15:52

Chama tawala cha Taiwan chashinda Urais kwa awamu ya tatu mfululizo


Wafuasi wa mshindi wa urais wa Taiwan, Lai Ching-te wakishangilia ushindi wake Jumamosi. Januari 13,2023.
Wafuasi wa mshindi wa urais wa Taiwan, Lai Ching-te wakishangilia ushindi wake Jumamosi. Januari 13,2023.

Chama tawala cha Taiwan cha Democratic Progressive, kimepata ushindi usiotarajiwa wa urais kwa awamu ya tatu mfululuzo  Jumamosi, huku mgombea wa chama wake, Makamu Rais wa sasa Lai Ching-te, akishinda kwa asilimia 40 ya kura.

Amemshinda Hou Yu-ih, mgombea urais wa chama cha upinzani cha Kuomitanga, au KMT chenye uhusiano wa karibu na China, na mkuu wa zamani wa polisi, pamoja na Ko Wen-je, mgombea urais wa Taiwan People’s Party, ambaye alijaribu kukiwasilisha chama chake kama mbadala vya vyama viwili vikuu.

Katika hotuba yake, Lai amesema ushindi wake wa Jumamosi ni ushindi wa demokrasia ya jumuiya ya kimataifa. “Tunaiambia jumuiya ya kimataifa kwamba kati ya demokrasia na ubabe, tutasimaa upande wa demokrasia,” alikiamba chumba ambacho kilikuwa na zaidi ya waandishi wa habari 100 wa ndani na nje ya Taiwan.

Forum

XS
SM
MD
LG