Msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha People’s Democratic Party nchini Nigeria amekanusha madai kwamba chama hicho kimemtoa kafara katibu wake wa mawasiliano kufuatia vita vya kupambana na ufisadi vilivyotangazwa na rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari.
Wiki mbili zilizopita, tume ya uhalifu wa kiuchumi na Fedha nchini Nigeria, EFCC, ilimkamata na kumfungulia mashitaka saba msemaji wa chama hicho OLISA METUH.
Hata hivyo, naibu msemaji wa kitaifa wa chama hicho, ABDULLAHI JALO, alisema chama cha DPP hakiwajibiki kwa shutuma anazokabiliwa nazo METUH na wengine, kwani fedha anazoshukiwa kuchukua hazikuwekwa kwenye akaunti za chama, bali zilienda kwenye akaunti binafsi.