Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:23

Chama cha Waziri Mkuu wa India na washirika wake wanatazamiwa kurejea mamlakani katika jimbo tajiri zaidi la taifa hilo

Wafuasi wa Chama cha Bharatiya Janata wakisheherekea huku waziri mkuu wa India Modi akiwasili kuwahutubia baada ya kushinda uchaguzi wa jimbo muhimu la kisiasa la India la Maharashtra, huko New Delhi, India, Jumamosi, Nov. 23 , 2024. (Picha na AP)

Chama cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na washirika wake wanatazamiwa kurejea mamlakani katika jimbo tajiri zaidi la taifa hilo

Chama cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na washirika wake wanatazamiwa kurejea mamlakani katika jimbo tajiri zaidi la taifa hilo, vituo vya televisheni viliripoti leo Jumamosi, ikiwa ni msukumo wa kutia moyo kwa kiongozi huyo wa Kihindu baada ya uchaguzi mkuu uliokatisha tamaa.

Huko Maharashtra makao makuu mji mkuu wa kifedha wa India Mumbai, muungano wa Mahayuti unaoongozwa na Chama cha Bharatiya Janata ulikuwa unaongoza kwa viti 221 kati ya 288. Chama cha upinzani cha Congress na washirika wake wanaongoza kwa viti 55 katika uchaguzi wa majimbo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Serikali ya Mahayuti imepata mafanikio yasiyopingika na makubwa, Eknath Shinde, waziri mkuu wa jimbo hilo, alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Forum

XS
SM
MD
LG