Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:28

Upinzani wa UDP nchini Gambia washinikiza kuachiliwa kwa kiongozi wao


Rais wa Gambia, Yahya Jammeh.
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh.

Naibu Rais wa chama kikuu cha upinzani cha Gambia cha United Democratic Party (UDP), Mariam Secka ameisihi jumuiya ya kimataifa kusaidia kushinikiza kuachiliwa kwa kiongozi wa chama hicho Ousaniou Darboe.

Darboe, pamoja na wanachama wengine 38 wa upinzani, walikamatwa mwezi uliopita na kufunguliwa mashtaka kwa kupanga njama za kutenda uhalifu. Awali walishtakiwa kwa makosa ya kukusanyika bila kibali, kafanya ghasia, na uchochezi wa kuzusha ghasia, baada ya mkutano wa kisiasa wakidai mabadiliko ya mfumo wa kisiasa, na kuandamana dhidi ya kifo cha afisa wa chama cha UDP, Solo Sandeng, aliyekufa akiwa kizuizini.

Jaji siku ya Alhamisi alikataa kumuachilia Darboe kwa dhamana. Naibu Katibu Mkuu wa chama cha UDP, Mariam Secka, amesema chama chake hakina Imani na sheria za Gambia ambazo, amesema, mara nyingi zinawajibika kwa Rais wa nchi hiyo, Yahya Jammeh.

XS
SM
MD
LG