Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:44

Chama cha Biden kimeshinda viti vingi katika senate


Rais wa Marekani Joe Biden akipanda ndege akiondoka Marekani kuelekea Misri, Cambodia na Indonesia Nov 10, 2022
Rais wa Marekani Joe Biden akipanda ndege akiondoka Marekani kuelekea Misri, Cambodia na Indonesia Nov 10, 2022

Chama cha democrat kimepata ushindi wa viti 50 na hivyo kuendelea kudhibiti baraza la senate, hatua inayompa ushindi mkubwa rais Joe Biden na kuzima matumiani ya “wimbi Jekundu” ambalo chama cha Republican kililitarajia kuelekea uchaguzi wa kati kati ya muhula nchini Marekani.

Biden ambaye amekuwa kipambana na viwango vya chini utendaji kazi wake kabla ya uchaguzi wa Jumanne kutokana na umma kufadhaishwa na mfumuko wa bei, amesema kwamba matokeo ya uchaguzi huo yanampa kuangalia mbele kwa kipindi chake kilichobaki madarakani.

Kiongozi wa walio wengi katika senate Chuck Schumer ameutaja ushindi wa chama cha democratic kama uthibitisho wa wamarekani kuwa na matumaini na utawala wa Biden.

Hata hivyo chama cha Republican kinakaribia kupata ushindi mwembamba katika baraza la wawakilishi. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea.

Kufikia sasa, warepublican wana viti 211 huku wademocrat wakiwa na viti 205. Mshindi anastahili kupata viti 218 katika bunge hilo lenye viti 435.

XS
SM
MD
LG