Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:49

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre, kuhukumiwa nchini Senegal


Rais wa zamanai wa Chad,Hissène Habré.
Rais wa zamanai wa Chad,Hissène Habré.

Hii ni mara ya kwanza duniani, kwa mujib wa shirika la Human Rights Watch, ambapo mahakama katika taifa moja limemfungulia mashtaka kiongozi wa zamani wa taifa jengine kwa tuhuma za ukiukaji wa haki za binadam.

Mahakama nchini Senegal inatarajiwa Jumatatu kutoa hukumu katika kesi dhidi ya dikteta wa zamani wa Chad, Hissene Habre.

Bw Habre alishtakiwa kwa shutuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu, mateso, na uhalifu wa kivita kwenye mahakama maalum mjini Dakar, Senegal, ijulikanao kama The extraordinary African Chambers.

Hukumu huwenda ikaadhimisha mwisho wa mapambano marefu ya kumfikisha Habre mbele ya sheria nchini Senegal, ambako alikimbilia na amekuwa akiishi uhamishoni baada ya kupinduliwa katika mapinduzi ya mwaka 1990.

Reed Brody wakili katika shirika la Human Rights Watch anasema, imechukuwa miaka 25 ya kampeni zisizosita zilizofanywa na waathirika wa Hissene Habre, kuhakikisha kesi inaendeshwa.

Mahakama hiyo ilimfungulia mashtaka rais wa zamani wa Chad mwaka 2013 na kumweka kizuizini akisubiria kesi. Baada ya uchunguzi wa miezi 19, mahakimu wanasema kuna ushahidi wa kutosha wa kuendesha kesi dhidi ya Habre.

Hii ni mara ya kwanza duniani, kwa mujib wa Human Rights Watch, ambapo mahakama katika taifa moja limemfungulia mashtaka kiongozi wa zamani wa taifa jengine kwa tuhuma za ukiukaji wa haki za binadam.

XS
SM
MD
LG