Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 05:51

Chad yakabiliwa na dharura ya chakula na lishe.


Rais wa Russia Vladmir Putin akutana na rais wa Senegal Macky Sall, SOCHI.

Rais wa mpito wa Chad Mahamat Idriss Deby ametia saini agizo la kutangaza dharura ya chakula na lishe. Anasema uamuzi huo unafuatia kuporomoka kwa hali ya chakula na lishe mwaka huu.

Rais wa mpito wa Chad Mahamat Idriss Deby ametia saini agizo la kutangaza dharura ya chakula na lishe.

Anasema uamuzi huo unafuatia kuporomoka kwa hali ya chakula na lishe mwaka huu , hali inayohatarisha wimbi kubwa la watu walio katika hatari kama msaada wa kibinadamu hautotolewa.

Ombi la msaada wa kibinadamu limekuja kabla ya mkutano baina ya mwenyekiti wa umoja wa Afrika Macky Sall na rais wa Russia Vladmir Putin kwa ajili ya kujadiliana kuhusu usambazaji wa nafaka wa Russia.

Umoja wa mataifa umeonya kwamba zaidi ya watu milioni 5.5 nchini Chad zaidi ya theluthi moja ya watu watahitaji msaada mwaka huu.

Shirika la chakula duniani limesema mwezi Machi takriban watu milioni 2.1 wa Chad watakumbwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula wakati wa msimu wa kipindi kikavu utakapoanza mwezi huu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG