Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:03

Chad yaidhinisha Deby kama rais wa mpito


Mahamat Idriss Deby akiapishwa kama rais wa mpito Jumatatu
Mahamat Idriss Deby akiapishwa kama rais wa mpito Jumatatu

Kiongozi wa baraza la kijeshi linaloongoza Chad Mahamat Idriss Deby leo amesema kwamba serikali ya muungano wa kitaifa itaundwa katika siku chache zijazo kwelekea kwenye uchaguzi mkuu, kufuatia mazungumzo ya kitaifa kuhusiana na hatma ya kisiasa ya taifa hilo.

Deby amesema hayo muda mfupi baada ya kuidhinishwa kama rais wa mpito, baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo mwishoni mwa wiki, huku akiahidi kwamba matarajio ya watu wa Chad yataheshimiwa. Bunge la taifa hilo lilivunjwa Jumapili, huku katiba pia ikisimamishwa, baada ya Deby kutangazwa kuwa rais wa mpito. Kabla ya kutangazwa kuwa rais wa mpito, Deby aliongoza baraza la kijeshi la majenerali 15, ambalo alisema limeongoza taifa hilo kwa miezi 18 sasa, na hivi sasa utawala wa mpito utaendelea kwa miezi mingine 18 ili kutayarisha katiba mpya na uchaguzi mkuu. Baadhi ya viongozi waliyohuduria hafla hiyo ni pamoja na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, mawaziri kutoka Niger, Jamhuri ya Afrika ya kati pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Mawaziri wa Ufaransa pamoja na EU pia walihudhuria.

XS
SM
MD
LG