Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:03

Chad yaanza kuondoa wanajeshi Mali


Wanajeshi wa Chad wakiwa na wakimbizi nchini Mali..
Wanajeshi wa Chad wakiwa na wakimbizi nchini Mali..
Chad imeanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Mali, ambako kwa miezi kadhaa wamekuwepo huko kusaidia kupambana na wanamgambo wa ki-islamu upande wa kaskazini mwa nchi.
Rais wa Chad, Idris Deby amesema wanajeshi wake wamekalimisha operesheni yao na hawataweza kupigana katika vita vinavyoibuka sasa nchini Mali.

Baada ya ufaransa kupeleka wanajeshi wa kutoa msaada katika upande wa kaskazini uliodhibitiwa na wanamgambo wa ki-islam, Chad pia ilipeleka wanajeshi 2,000 kuyasaidia majeshi ya Mali upande wa kaskazini mwa nchi.

Ufaransa imeondoa wanajeshi wake 100 wiki iliyopita ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuondoka nchini Mali.
XS
SM
MD
LG