Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:16

Chad: Watu watano wauawa katika maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi


Rais wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss Deby
Rais wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss Deby

Watu watano wameuawa leo Alhamisi wakati polisi wakikabiliana na waandamanaji katika mji mkuu wa Chad, N’Djamena, katika maandamano yaliyopigwa marufuku, dhidi ya utawala wa kijeshi .

Mamia ya waandamanaji wamejitokeza kuadhimisha tarehe ambapo jeshi lilikuwa limeahidi awali kukabidhi madaraka, muda huo sasa umeongezwa kwa miaka miwili zaidi.

Mwandishi wa AFP aliona miili mitano kwenye sakafu ya hospitali ya jiji, Union Chagoua Hospital, miwili ikiwa imefunikwa na bendera ya taifa ya Chad, na mitatu ikiwa na shuka nyeupe zilizojaa damu.

Daktari mkuu wa hospitali hiyo, Joseph Ampil, ameithibitishia baadaye AFP kwamba watu watano walifariki kutokana na majera ya risasi za bunduki, wakati wa makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.

XS
SM
MD
LG