Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:55

Chad: Watu 11 wanaoshtumiwa kupanga njama ya mapinduzi wahukumiwa miaka 20 jela, Rais aahidi kuwasamehe


Rais wa Chad Jenerali Mahmat Idriss Deby Itno.
Rais wa Chad Jenerali Mahmat Idriss Deby Itno.

Watu 11 wanaoshutumiwa kupanga mapinduzi nchini Chad wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, mwanasheria mkuu mjini N’Djamena ameliambia shirika la habari la AFP Jumapili, lakini ofisi ya rais imesema watasamehewa.

Mapema mwezi Januari, serikali ilitangaza kwamba maafisa 10 wa jeshi na mwanaharati maarufu wa haki za binadamu Berdei Targuio walikamatwa wakishtumiwa “kujaribu kuvuruga utaratibu wa kikatiba” na taasisi za nchi.

Berdei Targuio aliyetambulishwa na mamlaka kama kiongozi wa mpango huo wa kufanya mapinduzi mwezi Disemba, ni mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu la Chad (OTDH) na mkosoaji mkubwa wa utawala.

Watu 11, ambao wamezuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali la Koro Toro, kwenye umbali wa kilomita 600 kaskazini mwa mji mkuu, walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuvunja utaratibu wa kikatiba, kumiliki silaha kinyume cha sheria na kushirikiana na wahalifu, kulingana na shirika la habari la taifa.

Tarehe 21 Aprili, Rais wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno aliapa kuwaachia huru.

“Rais atatekeleza ahadi yake,” msemaji wa ikulu Brah Mahamat ameiambia AFP, akiongeza kwamba lazima hukumu itangazwe kabla ya msamaha wa rais kutolewa.

Deby alichukuwa madaraka baaada ya baba yake, rais Idriss Deby Itno, ambaye alitawala kwa miaka 30, kufariki wakati wa operesheni dhidi ya waasi mwezi Aprili mwaka wa 2021.

XS
SM
MD
LG