Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:38

Chad na Cameroon wapambana na Boko Haram


Picha ya maktaba, inayoonyesha wanajeshi wa Chad.
Picha ya maktaba, inayoonyesha wanajeshi wa Chad.

Mamia ya wapiganaji wa Boko Haram, wamevuka mpaka kuingia Cameroon Jumatano, kupambana na wanajeshi wa Chad na Cameroon.

Wanajeshi wa nchi hizo mbili walipelekwa kupambana na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi kutoka Nigeria.

Mashuhuda wanasema wapiganaji waliingia katika mji wa Fotocol, katika mpaka wa Nigeria na Cameroon na kushambulia wanajeshi wa Chad.

Inaripotiwa kwamba mapigano makubwa yalizuka baina ya pande zilizokuwa zinapigana.

Serikali ya Chad imesema majeshi yake yalipambana na mashambulizi ya Boko Haram, katika mji wa Fotocol, siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa Chad, wanajeshi wake waliwakimbiza wanamgambo hao katika mji wa Nigeria, wa Gambaru.

Chad inasema imewaua zaidi ya wanamgambo 200 wa Boko Haram, na wao kupoteza wanajeshi tisa.

Hakuna uthibitisho huru kuhusu idadi ya waliouliwa.

XS
SM
MD
LG