Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 19:08

Serikali ya Chad yazuia mitandao ya kijamii


Kwa zaidi ya miezi mitatu sasa imekuwa ni vigumu kupata mitandao ya kijamii nchini Chad. Baadhi ya watumiaji wa kawaida wa mtandao wanasema wameweza kuepuka vizuizi kwa kutumia program za kompyuta, lakini wamelalamikia hujuma ya kile walichokisema hatua ya serekali kuzuia uhuru wa kujieleza.

Wakosoaji wanasema hatua hiyo ni ya makusudi ya utawala wa rais Idriss Deby kuzuia kupashana habari kuhusu masuala muhimu, kama ya ubakaji wa wasichana wadogo ambalo limeshtua jumuiya ya kimataifa na uchaguzi wa hivi karibuni wa nchini humo.

Serikali ya Chad haijazungumza chochote kuhusiana na shutuma hizo na VOA ilipowasiliana na waziri wa mawasiliano kuhusu taarifa hizi hakujibu chochote.

XS
SM
MD
LG