Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 08:08

Chad: Idriss Deby Itno aahidi kuunda "serikali ya umoja wa kitaifa"


Rais wa Chad Idriss Deby akiwasalimia wafuasi wake wa Patriotic Salvation Movement wakati wa mkutano katika mji mkuu N'djamena.

Kiongozi  wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno, Jumatatu alisema "serikali ya umoja wa kitaifa" itaundwa katika siku zijazo, ili kuongoza awamu ya kuelekea uchaguzi mpya kufuatia kongamano kuhusu mustakabali wa nchi hiyo lililofanyika Jumamosi.

Chad, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, imekumbwa na misukosuko ya mara kwa mara na machafuko tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.

Deby, jenerali wa nyota tano mwenye umri wa miaka 38, alichukua usukani Aprili 2021, baada ya babake, Idriss Deby Itno, ambaye alikuwa ametawala kwa mabavu kwa miongo mitatu, kuuawa wakati wa operesheni dhidi ya waasi.

Bunge lilivunjwa na katiba ikasimamishwa na Deby akatangazwa kuwa rais. Aliongoza jopo la kijeshi la majenerali 15, ambapo mpango wao uliotangazwa ulikuwa wa kukabidhi madaraka baada ya miezi 18 -- muda ambao ungemalizika mwezi huu. Deby kisha akaandaa "mazungumzo jumuishi ya kitaifa" ambayo alisema yangepanga kurejea kwa nchi katika utawala wa kiraia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG