Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 12:29

CDC yatabiri watu wengi wataambukizwa Ebola Afrika magharibi


Mfanyakazi wa WHO akiwapa mafunzo wauguzi wa afya huko Freetown, Sierra Leone, Septemba 18,2014

Watafiti wa Marekani wanasema kati ya watu 500,000 na milioni 1.4 katika nchi za Afrika magharibi wataweza kuambukizwa ugonjwa wa Ebola ifikapo mwezi Januari ikiwa janga hilo halitadhibitiwa . Wakati huo huo serikali ya Guinea inasema inapeleka vijana 2,000 kutembelea nyumba moja hadi nyingine ili kuelimisha familia kuhusu ugonjwa wa Ebola kufuatia mauwaji yaliyofanyika wiki iliyopita.

Utabiri kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani-CDC unatokana na mtazamo ambao unachukulia kwamba idadi ya watu wanaoambukizwa na virusi pamoja na kesi zinaongezeka mara mbili kila baada ya wiki kadhaa nchini Liberia na Sierra Leone na kwamba idadi ya kesi hivi sasa zilizoripotiwa na shirika la afya duniani-WHO ni ndogo mno.

CDC inaeleza kwamba utabiri wake mkubwa huwenda usitendeke mara baada ya juhudi mpya za kupambana na Ebola kutekelezwa ikiwemo kuongeza vituo vya matibabu na Marekani kuahidi kupeleka wanajeshi 3,000 kwenye kanda iliyoathiriwa.

Wafanyakazi wa afya wakibeba maiti iliyotokana na ugonjwa wa Ebola
Wafanyakazi wa afya wakibeba maiti iliyotokana na ugonjwa wa Ebola

Shirika lilisema mlipuko huo unaweza kudhibitiwa kama asilimia 70 ya wagonjwa wanawekwa katika vituo ambako hatari ya uambukizaji inapunguka.

Wakati huo huo huko Guinea serikali imeanza juhudi za kuelimisha wakazi kufuatia mauaji ya watu wanane waliokuwa wakisafiri huko kusini-mashariki kama sehemu ya msafara wa serikali wa kuongeza mwamko kuhusu virusi hivyo.

Serikali ya Guinea inasema kile kilichotokea katika kijiji cha Wome wiki iliyopita lazima kisitokee tena.

Wanavijiji walishambulia msafara wa maafisa hao wa serikali na kuwauwa watu wanane walokua wanasafiri kwenda kuelimisha watu juu ya hatari za Ebola

Msemaji wa serikali Albert Damatang Camara aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba watu 20 wamekamatwa na uchunguzi unaendelea. Pia anasema wanafanya mabadiliko kwenye mkakati wao wa Ebola.

XS
SM
MD
LG