Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:36

CDC yasema matibabu ya Ebola yanafanikiwa

Dr.Kent Brantly wa Marekani akihudumia wagonjwa wa Ebola hapo awali, ameambukizwa maradhi hayo.
Dr.Kent Brantly wa Marekani akihudumia wagonjwa wa Ebola hapo awali, ameambukizwa maradhi hayo.

Katika siku za nyuma kirusi cha Ebola kilichosambaa katika nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia kiliripotiwa kuuwa asilimia 90 ya wote walioambukizwa.

CDC yasema matibabu ya Ebola yanafanikiwa

Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi umesababisha vifo vya watu 670 na kuambukiza wengine 1,200. Lakini mtaalam wa idara ya Marekani ya kuzuia na kudhibiti magonjwa anasema wengine wengi wataambukizwa katika wiki na miezi ijayo.

Idara hiyo ya Marekani ya kuzuia na kudhibiti magonjwa ,CDC inapuuzilia wasiwasi wa uwezekano wa maambukizo ya kirusi cha Ebola Marekani kwa sababu ya namna hospitali za Marekani zinavyofanya kazi kuzuia maambukizo.

Wafanyakazi wawili wa afya raia wa Marekani waliokuwa wakifanya kazi Afrika Magharibi wameambukizwa maradhi hayo.

Katika siku za nyuma kirusi cha Ebola kilichosambaa katika nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia kiliripotiwa kuuwa asilimia 90 ya wote walioambukizwa.

CDC inasema kwa sasa kirusi hicho kimeambukiza asilimia 60 ya watu, idadi ambayo wataalam wanasema inaonyesha matibabu yanafanya kazi.

XS
SM
MD
LG