Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:26

C.A.R. yapata waziri mkuu mpya


Rais wa C.A.R. Catherine Samba-Panza
Rais wa C.A.R. Catherine Samba-Panza

Mahamat Kamoun mwenye umri wa miaka 53 ni muislam wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu katika C.A.R. tangu ilipopata uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1960

Jamhuri ya Afrika ya Kati- C.A.R. imepata waziri mkuu wake wa kwanza muislam.

Mahamat Kamoun, mashauri wa zamani wa masuala maalumu kwa rais wa mpito, Catherine Samba-Panza, ataongoza serikali ya mpito ambayo inataka hatua zichukuliwe haraka kutekeleza mkataba wa kusitisha mapigano uliotiwa saini mwezi uliopita baada ya mwaka mmoja wa ghasia za kidini.

Bwana Kamoun mwenye umri wa miaka 53 aliteuliwa na rais Samba. Kamoun ni muislam wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu katika C.A.R tangu ilipopata uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1960.

Alikuwa mkurugenzi mkuu wa fedha chini ya rais wa zamani Francois Bozize. Pamoja na bibi Samba-Panza ambaye ni mkristo, bwana Kamoun anakabiliwa na kazi ngumu ya kusimamia mazungumzo tete ya mpito wa kisiasa yanayolenga kumaliza ghasia za kidini ambazo zimesababisha maafa makubwa nchini humo.

XS
SM
MD
LG