Rais wa FIFA Gianni Infantino alitangaza uamuzi huo katika mkutano mkuu wa Shirikisho hilo Jumatano nchini Moscow.
“Kwa hivyo tunaye mshindi, kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 wanachama wa jumuiya za Canada, Mexico na Marekani wamechaguliwa na mkutano mkuu wa FIFA kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA, asanteni.’
Nchi wanachama wa FIFA walipiga kura 134 dhidi ya kura 65 kuunga mkono kundi la mataifa matatu dhidi ya Morocco, taifa pekee la Afrika lililokuwa katika kinyang'anyiro hicho.
Marekani itakuwa wenyeji wa mechi 60 kuchezea katika viwanja vyake kati ya 80 katika michezo iliyopangwa, wakati Mexico na Canada watakuwa wenyeji wa mechi zilizobakia.
Michuano hiyo ya Kombe la Dunia 2026 itakuwa ni ya kwanza kuongeza idadi ya timu kufikia 48, kutoka idadi iliyoko sasa ya timu 32.
Michuano ya Kombe la Dunia 2018 itaanza Alhamisi na Wenyeji wa mashindano hayo Russia wakicheza na Saudi Arabia. Michuano ya 2022 itafanyika Qatar.
Facebook Forum