Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 26, 2025 Local time: 22:02

Canada imezindua mpango wa uhamiaji kuvutia wataalamu wenye ujuzi


H-1B Visa, ni Visa kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni na wenye ujuzi
H-1B Visa, ni Visa kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni na wenye ujuzi

H-1B visa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni wasio wahamiaji na wenye ujuzi maalum wanaoishi nchini Marekani.

Kuanzia Julai 16 watu hadi 10,000 wenye visa za aina hiyo wanaweza kuomba kufanya kazi nchini Canada. Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpya nchini humo wa Tech Talent Strategy.

“Serikali ya Canada inakumbatia jukumu linalojitokeza la Canada kuwa kama kiongozi katika kuajiri wenye vipaji vya teknolojia na pia kuwa kivutio ili kuhakikisha Canada siyo tu inajaza kazi zinazohitajika leo, lakini pia kuvutia ujuzi na vipaji vya biashara ili kubuni ajira za kesho,” taarifa iliyotolewa na idara ya Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia Canada ilisema.

Hii inafuatia tangazo la Novemba ambapo serikali iliweka lengo la kukabiliana na uhaba wa ajira. Ifikapo mwaka 2025, Canada inataka kuwakaribisha wahamiaji milioni 1.45 ikiwalenga watu waliosomea katika fani za huduma za afya na stadi nyingine za ajira zinazohitajika, na kupata wafanyakazi wenye ujuzi kwenye sekta muhimu za uchumi wake.

Forum

XS
SM
MD
LG