Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema atajiuzulu rasmi Jumatano ili kumpisha waziri wa mambo ya ndani Theresa May kuwa kiongozi wa nchi hiyo.
Cameron amesema Jumatano atajibu maswali kutoka kwa wajumbe wa baraza kuu la Bunge. Baada ya hapo Cameron amesema atapeleka barua ya kujiuzulu kwenye ikulu ya kifalme ili kumpisha waziri mwingine mkuu kufikia Jumatano jioni.
May pamoja na waziri wa nishati Andrea Leadsom walitarajiwa kushindana kwenye mchujo wa chama cha Conservertive ili kuchukua nafasi ya Cameron alietangaza kujiuzulu baada ya kushindwa kuwashawishi wapiga kura wa Uingereza kubaki kwenye muungano wa Ulaya katika kura iliopigwa mwezi uliopita.
Hata hivyo Leadson jumatatu alitangaza kujiondoa na kwa hivyo kuwacha May akiwa mgombea pekee atakechukua wadhifa wa Cameron.