Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:04

Madaktari wametishia kugoma Tanzania


Zahanati ya wanawake wanaougua baada ya upasuaji Tanzania
Zahanati ya wanawake wanaougua baada ya upasuaji Tanzania

Chama hicho cha madaktari pia kilimfuta uanachama Mganga Mkuu wa serikali

Serikali ya Tanzania Jumanne kimepuuzilia mbali onyo lilitolewa na chama cha madaktari kilichotoa muda wa saa 78 kwa Serikali hiyo kuwarejesha kazini madaktari kadhaa ambao walisimamishwa toka kwenye vituo vyao vya kazi.

Chama hicho cha madaktari pia kilimfuta uanachama Mganga Mkuu wa serikali kwa madai kuwa ameshindwa kutekeleza vyema majukumu yake kwa kuegemea zaidi upande wa Serikali.

Chama hicho kinailaumu Serikali kwa kushindwa kuwakirimu ipasavyo madakatari kadhaa ambao kinasema kuwa kimsingi wanapaswa kupewa dhamana yote ya kiutalamu tofauti na ilivyo sasa ambavyo serikali inawaona kama wanafunzi walioko kazini kwa ajili ya mazoezi ya vitendo.

Kauli hiyo iliwakwaza madaktari waliko katika hospitali ya taifa Muhimbili na kutishia kuanzisha mgomo iwapo Serikali itaendelea kukaidi zingatio lililowekwa na wataalamu hao a afya.

Hata hivyo ikiwa imepita saa 24 tangu kutolewa kwa onyo hilo kwa Serikali, hali inavyoonekana sasa kila sehemu unavuta kamba upande wake. Kulingana na maelezo yaliyotolewa na Naibu waziri wa afya na Ustawi wa Jamii Dr Lucy Nkya, Serikali kamwe haiku tayari kusalim amri kwa madakatari hao.

Kuanza kwa vuta nikuvute hiyo kunatokana na hatua ya Serikali kuwacheleweshea mishahara madaktari hao ambao wanadai kuwa Serikali haitoi kipaumbele kipasacho kwa sekta hiyo na wafanyakazi wake.

Kutokana na hali hiyo kuliwasukuma madaktari kadhaa kuingilia mgomo ambao ulipata msukumo mkubwa baada ya kuungwa mkono na madaktari kadhaa waliopo katika hospitali ya taifa ya muhimbili na ile iliyoko mkoani Dodoma.

XS
SM
MD
LG